Loading...
 

Mashindano ya Kusimulia Hadithi

 

Narrative 794978 960 720

 

Muda wa Hotuba

Mashindano ya Kusimulia Hadithi yana lengo la kutafuta wabunifu na wasimulizi wa hadithi bora ambao wanaweza kuburudisha, kusukuma, na kufundisha watu.

Hotuba zinazoingia kwenye Mashindano ya Kusimulia Hadithi lazima ziwe na muda wa usiozidi dakika 10.

Hadithi zinaweza kujumuisha ucheshi/vichekesho, lakini zisiwe tu kuhusu ucheshi/vichekesho.

Uchaguzi wa Majaji

Kwa mashindano ya ngazi ya nchi na juu, majaji watakuwa sio wanachama wa Agora, ambao watakuwa kutoka taalum zifuatazo:

  • Wataalam wa vyombo vya habari - watangazaji, watangazaji wa vipindi, waigizaji, watayarishaji, nk., kutoka runinga, redio, magazeti, au filamu.
  • Waandishi wa hadithi za kubuni
  • Waandishi wa habari
  • Wazungumzaji wataalam kutoka mzunguko wa wazungumzaji wa mbele ya hadhira (wanaolipwa).
  • Wazungumzaji kutoka matukio mengine ya uzungumzaji wa mbele ya hadhira kama vile TEDx., Munk Debates, nk.


Alama za Hotuba

Majaji watatoa alama za hotuba kulingana na vigezo vifuatavyo:

  • Uhalisia (0 mpaka 10) - Watazingatia hadithi ina uhalisia gani.
  • Maendeleo ya hadithi (0 mpaka 10) - Watazingatia hadithi kwa ujumla, utambulisho, maendeleo, kilele, nk.
  • Maendeleo ya wahusika (0 mpaka 10) - Watazingatia kama mhusika mkuu wa hadithi alikuwa na utambulisho unaofaa na wa kina, maendeleo, na hitimisho.
  • Utumiaji wa lugha (0 mpaka 10) - Watazingatia utajiri, maelezo, na uwazi wa lugha ambayo imetumiwa. Uwezo wa mzungumzaji kujenga picha kwenye akili za hadhira.
  • Ubora wa masimulizi (0 mpaka 10) - Watazingatia utofauti wa sauti, lugha ya mwili, mapumziko, na sifa nyingine za usimulizi.
  • Uwepo wa hisia (0 mpaka 10) - Watazingatia uwezo wa msimulizi wa hadithi kufikisha na kuchochea hisia kwa hadhira.
  • Ujumbe wa hadithi (0 mpaka 10)- Watazingatia ujumbe wa msingi wa kimaadili wa hadithi.

Kwa kila hotuba, wastani wa kila alama za hapo juu utatafutwa, na hiyo ndio itakuwa alama ya mwisho atakayopewa mshiriki.

Cheo

Mshindi wa ngazi yoyote isipokuwa Fainali za Dunia atakuwa na cheo cha "Msimulizi Bora wa Hadithi wa (kanda)"


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Saturday August 21, 2021 08:28:46 CEST by zahra.ak.